Mwongozo wa Wapiga Kura

Vidokezo 7 vya Kusafisha Taarifa Zako

Pakua mwongozo huu kama PDF

Sehemu hii ya kifaa cha kusafisha taarifa inachunguza yafuatayo:

  • Ni kwa namna gani kampeni za kisiasa zinatumia taarifa zangu kunihamasisha?
  • Ni mahali gani ambapo kampeni zinapata taarifa zangu?
  • Je, akaunti zangu za mitandao ya kijamii zinasema nini kunihusu?
  • Je nilikubali kuchangia taarifa zangu / maudhui yangu?
  • Ni kwa jinsi gani matangazo ya kisiasa yananilenga mimi?
  • Ni kwa namna gani waendesha kampeni wanajua msimamo wangu?
  • Nifanye nini sasa?

Ngoja tuanzie hapa sasa!


Ni jinsi gani kampeni za kisiasa zinatumia taarifa zangu kunishawishi?

Inawezekana unaona matangazo ya kisiasa kila mahali; kutoka kwenye tovuti una zotembelea, mitandao ya kijamii, na vipeperushi mlangoni pako. Inawezekana kila mtu anaongelea masuala muhimu kwako. Na sio kwa bahati mbaya.

Kampeni za Kisiasa zinavyozidi kukufahamu zaidi, ndivyo zinavyoongeza ushawishi juu yako - iwe ni kwa kushiriki katika kazi za kujitolea, kukushawishi kuchangia, kushawishi kupiga kura au kukufanya kufika katika kituo cha kupiga kura siku ya uchaguzi.

Bahati yao, taarifa kukuhusu na jinsi ya kukulenga ni rahisi kupata. Matangazo ya kisiasa yanaongozwa na taarifa unazoacha mtandaoni na nje ya mtandao. Kampeni za kisiasa zinakusanya taarifa hizi kwa njia mbalimbali na kutengeneza wasifu kukuhusu. Wasifu huu unawasaidia kutengeneza ujumbe maalum kukuhusu.

Kulingana na wasifu wako, kampeni inaweza kutuma jumbe binafsi za siasa kwa njia ya:

  • vipeperushi nyumbani
  • zana binafsi ya kuhariri picha ya Snapchat
  • upakuaji wa haraka programu za kampeni
  • matangazo kwa njia ya YouTube au runinga janja
  • barua pepe, jumbe za simu au kupiga simu
  • toleo la tovuti ya mgombea

Inawezekana unadhani kuwa: 'Je, matangazo mahususi na yanayofaa si bora kwangu?' Zingatia akilini ya kuwa kampeni za kidijitali zinaweza kutumia taarifa za faragha za tabia na maslahi yako. Hii inaweza kuhusisha taarifa ambazo si za kisiasa kama tovuti unazotembelea au manunuzi yako.

Una haki ya kujua jinsi taarifa zako zinavyotumika, hasa ikiwa zinatumika kushawishi au kuchochea kabla ya uchaguzi. Tactical Tech wamefanya uchunguzi kuhusu mbinu maarufu za kampeni zinazoendeshwa na taarifa ili kuwafikia, kuwakagua, na kuwashawishi wapiga kura kwenye uchaguzi duniani kote.

Mwongozo wa Kifaa cha Kusafisha Taarifa kwa Wapiga Kura unaelezea baadhi ya mbinu mashuhuri zinazotumiwa na wagombea kupata msaada wa kupiga kura, maarifa ya jinsi na wakati gani wa kutumia mbinu za ushawishi.


Je, ni wapi waendesha kampeni wanatoa taarifa zangu?

Wanasiasa, Vyama vya siasa, na waendesha kampeni za kisiasa wanavutiwa kwako na shauku na tabia yako ya matumizi, mtindo wako wa maisha, na shughuli zako za mtandaoni, na mengine mengi. Je, ni kwa jinsi gani wanapata nafasi ya kufikia hizi taarifa?

Makampuni Makubwa ya Tehama (Teknolojia)

Makampuni kama Google na Facebook ni malango makuu ya kufikia taarifa zako kwa ajili ya vyama vya kisiasa.. Google na Facebook zimetawala viwanda / tasnia ya kidigitali ya matangazo kwa sababu wana taarifa nyingi za mabilioni ya watumiaji. Utajiri huu wa taarifa unamaanisha kwamba wateja wanaotaka kutangaza kupitia Google au Facebook - wakiwemo wanasiasa na vyama vya siasa - wanaweza kununua matangazo ambayo yanalenga hadhira wanayo ihitaji. Vyama vya siasa na wagombea wanatumia bajeti kubwa katika haya ‘yanayolenga’ wahusika mahususi.

Mawakala wa Taarifa na washauri wa siasa.

Waendesha kampeni pia wanaweza kupata taarifa zako kwa kununua kutoka kwa mawakala wa taarifa. Hizi ni kampuni kubwa za data ambazo zinamiliki data muhimu kwa undani za mamilioni ya watu duniani. Wanasiasa wanaweza kutumia taarifa hizi ili kuweza kujua taarifa zaidi kuhusu wafuasi wao ama wapiga kura muhimu. Mbali na Mawakala wa maudhui, washauri wa siasa wanaweza pia kufanya kampeni katika mfumo au muundo wao wa taarifa uliowekwa kwa ajili ya wapiga kura.

Vyanzo Vingine

Kampeni za kisiasa pia zinaweza kupata taarifa zinazowahusu wapiga kura kutokana na vyanzo mbalimbali kama vile:

  • rekodi za usaili za wapiga kura
  • hifadhidata himili
  • kura za maoni pamoja na tafiti zinazofanywa kupitia simu ya kiganjani.
  • rekodi za kiserikali za waliojitokeza pamoja na wagombea walioshinda katika chaguzi zilizopita katika maeneo yako husikaa.

Hata vitu kama vile mahali unaponunua, nini unachonunua, vitu unavyochapisha kwenye mitandao yako ya kijamii, kiwango chako cha kifedha , pamoja na kiwango chako cha elimu kinawapa nafasi wanasiasa kukujua vizuri na jinsi ya kukufikia.

KIDOKEZO CHA 1. Badilisha Ratiba Zako

Iwapo tabia zako kama mtumiaji zina umuhimu kwenye kampeni za kisiasa, kwanini usizichanganye? Unaweza ukaipumzisha kadi yako ya uaminifu,mara kwa mara lipia kwa fedha taslimu kwenye maduka ya mitaani au ufikirie mara mbili kabla ya kutoa namba za simu na taarifa zako binafsi.

Iwapo ungependelea kuvinjari jinsi taarifa za watumiaji zinatumika kuendesha kampeni za siasa, soma makala haya.


Mitandao Yangu ya Kijamii Inasema Nini Kunihusu?

Je, ulichapisha tweet kuhusu mabadiliko ya tabianchi? Je unatumia alama za mshangao katika kurasa za Facebook kuonyesha kushangawazwa? Hizi taarifa zinaweza kuonekana kama hazina madhara, lakini zinatoa taarifa nyingi kukuhusu kwa vyama vya siasa vinavyotaka kukufikia. Kwa kuchambua taarifa zako katika mitandao ya kijamii, makampuni yanaweza kufahamu ni maudhui gani yanaweza kuleta mabadiliko ya kihisia zako - iwapo unapenda maudhui ya kuhuzunisha, rangi ya buluu au chungwa, au kuhusu unavyohisi kuhusu swala fulani.

Mbinu hii inatumika kutambua kitu gani unapendelea na unachokisema mtandaoni (na jinsi unavyokisema) inaitwa usikilizaji wa kidigitali. ‘Kusikiliza’ watu katika mitandao ya kijamii kunaweza kusaidia wagombea kujua jamii inafikiri nini kuwahusu. Inaweza kusaidia kampeni kuchambua maswala ambayo wapiga kura wanayajali, na kutambua wachochezi wa siasa na watengenezaji simulizi za siasa.

Baada kuchambua watu wanasema nini kwenye mtandao wa Twitter kuanzia musuada wa Brexit hadi bangi, kampeni inaweza, kwa mfano, tengeneza jumbe tatu: mmoja kuwalenga wale ambao wamechoka kukiongelea kitu, na mwingine kwa wale wenye maoni yenye msimamo mkali kwa namna moja au nyingine.

Njia nyingine ambayo kampeni zinaweza kukusanya taarifa zako mtandaoni, ni kwa kutumia njia mbalimbali za matangazo na barua pepe. Hii inajulikana kama kipimo A/B. Wapiga kampeni wanaweza kuchambua maudhui yapi, rangi zipi na vichwa vya habari vipi vinavyohamasisha kuchangia, kupenda au kusambaza kwenye mitandao yako ya kijamii.

Makampuni au mashirika mara zote hayako wazi kuhusu iwapo yanafuatilia mienendo ya mitandao ya kijamiii, inafanya ugumu kujua kama unasikilizwa. Unapaswa hata hivyo, kudhani kuwa kwa kuongea katika hadhara za kidijitali kama Twitter au kurasa za Facebook au kuchangia katika makundi ya kurasa za Facebook, machapisho yako na majibu yanaweza kutumika kuelewa masuala ya kisiasa unayotaka kuongelea au hisia zako kuhusu suala.

KIDOKEZO CHA 2: Geuza Mapendeleo Yako Ya Mitandao ya Kijamii

Kuna hatua chache unazoweza kuchukua katika majukwaa ya mitandao ya kijamii ili kupunguza matumizi ya taarifa katika kutengeneza matangazo ya siasa unayopokea.

Angalia wasifu wako na mipangilio ili kubadili matangazo na chaguzi za masoko au kufuta historia ya shughuli zako katika majukwaa mbalimbali ili kupunguza uunganishaji katika shughuli za mtandaoni.

Soma “Karabati Wasifu Wako Wa Mtandao wa Kijamii” ili kujifunza zaidi.


Je, nakubali kushiriki taarifa zangu?

Vyama vya siasa vinapaswa kuomba ruhusa kabla ya kukusanya taarifa binafsi. lakini unapobofya ‘Nakubali’ kwenye tovuti, programu au kijarida, inaweza isiwe wazi kuhusu taarifa zipi za msingi unazokubali kuzitoa.

Uchapishaji mdogo wa sheria za faragha au tahadhari ambazo hazieleweki au zimefichwa zinaweza zikaleta ugumu kwenya kujua ni taarifa zipi zimekusanywa na jinsi zinavyotumika.

Unaweza ukawa unapata matangazo ya aina moja kila mahali mtandaoni. Sio sadfa! Makampuni yanatumia muunganiko wa kuki na programu za kufuatilia (pamoja na zana nyinginezo) ili kufuatilia watumiaji wanapoperuzi taarifa mtandaoni au kupata taarifa kwenye simu. Zana hizi zinaruhusu watangazaji kukushawishi kwa kukulenga na matangazo.

Chama cha kisiasa kinaweza kufuata mbofyo wako kwenye tangazo lao la Facebook linalounganisha na tovuti yao, kwa mfano, na kisha kuona ni sehemu gani za tovuti unazotembelea, kama vile sera zao za elimu au kurasa za michango. Kwa kutumia taarifa hii, wanaweza kukulenga na tangazo kulingana na maudhui hayo, na tangazo hilo hilo litatokea kwenye tovuti tofauti na zile unazoziperuzi.

Wakati mashirika yanaendesha tovuti yanatakiwa kuomba ridhaa yako kufanya hivyo, mara nyingi unabofya ‘kubali cookies zote’ kwa sababu hiyo ndio njia ya haraka kupata taarifa kwenye mtandao. kwa kufanya hivyo unaweza kupoteza mwongozo wa jinsi taarifa zako za msingi zinavyotumika.

KIDOKEZO CHA 3. Funga Kivinjari Chako cha Simu na Kompyuta ya Mezani

Ili kuweza kuwatangulia baadhi ya wafuatiliaji wa mtandaoni wanaotumiwa na vyama vya siasa:

  • Tumia njia za faragha kuperuzi pale inapowezekana
  • Sakinisha nyongeza ya viperuzi kama vile Privacy Badger na uwezeshe asili ili kufungia wafuatiliaji. (Kwa maana hizi ni nyongeza za viperuzi, bado utaweza kuona matangazo yanayokulenga kwenye programu unazotumia.)
  • Wezesha “Usinifuatilie” kwenye mipangilio yako ya simu. Tovuti hazihitajiki kuzingatia hili, lakini inatoa ishara kuwa haupendezwi na kufuatiliwa.
  • Tumia rasilimali zingine za Kifaa Cha Kusafisha Taarifa ili kuweza kudhibiti ufuatiliaji wa programu za matangazo.

Ni kwa vipi matangazo ya kisiasa yanalengwa kwangu?

Mitandao ya kijamii ina ufikiaji wa kila aina ya taarifa inayoweza kuwa muhimu kuhusu wapigakura, na hii inawafanya kuwa mahali pazuri kwa kampeni za kisiasa kufanya matangazo. Kampeni za kisiasa zinaweza kutumia Facebook (ambayo inamiliki Instagram), Google (ambayo inamiliki Youtube na Google Search), pamoja na Snapchat ili kuweza kukulenga pamoja na matangazo mahususi kulingana na vitengo kama umri wako, eneo unaloishi, na jinsia. Lakini wanaweza pia kutumia taarifa muhimu kama vile ni aina gani ya maudhui unayoweza kushiriki kwenye majukwaa yao, ikiwemo kama ‘kupenda’ na kutoa maoni yako.*

Kwa kuongezea, majukwaa ya mitandao ya kijamii hutoa huduma maalum mahususi kwa kampeni za kisiasa. Huenda hujui kuwa Facebook huruhusu kampeni za kisiasa kupakia orodha zao za wapigakura kwenye Facebook ili waweze kutuma matangazo ya kibinafsi kwa watu walio kwenye orodha hizo. Zaidi ya hayo, Facebook huwawezesha watangazaji wa kisiasa kulenga watu walio na wasifu sawa na wapiga kura kwenye orodha zao.

Facebook vilevile imesaidia kampeni za kisiasa kulenga zaidi matangazo yao kwa watumiaji wa mtandao. Kisa cha Cambridge Analytica kinachoonesha ni kwa vipi taarifa zinazotumika kwa uwezo mkubwa sana kwenye Facebook kuweza kupangilia wasifu wa wapiga kura kutokana na jinsi walivyo na uwazi,ufahamu wao,ubashashi wao,na vile wanavyofikiria. Wakati watu wengi wamesikia kuhusu Ccambridge Analytica, mbinu hii, na nyinginezo kama hizi, zinatumiwa pia na kampuni mbalimbali ili kuonesha malelezo yako kama mtumiaji au mpiga kura.

*Kumbuka: Kufikia Novemba 2019, makampuni mengi sana yakiwemo Facebook, Twitter, na Google yanarekebisha sera zao hasa kwenye matangazo ya kisiasa kwenye majukwaa yao.

KIDOKEZO CHA 4: Endelea Kupashika

Ili kupata maarifa zaidi kuhusu mandhari ya matangazo ya kisiasa, unaweza kuangalia:

Unaweza kutumia nyenzo hizi ili kuona ni kiasi gani cha pesa ambacho kampeni zilitumia na kwa matangazo yapi, katika maeneo gani, na pia maelezo ya msingi ya upangaji wa idadi ya watu. Zana hizi za uwazi, hata hivyo, bado hazipatikani katika nchi zote ambapo matangazo ya kisiasa yanahimiliwa.

Unaweza pia kuperuzi mradi wa Ad.Watch pambao hutoa mtazamo tofauti kwenye Maktaba ya Matangazo ya Facebook, au zingatia kusakinisha kiendelezi cha Who Targets Me ili kusaidia umati wa watu kupata matangazo ya kisiasa kwenye Facebook.


Je! Kampeni Zinajuaje Msimamo wangu (Kiuhalisia)?

Eneo lako linasema mengi kukuhusu. Kujua tu ni jiji gani na mtaa unaoishi kunaweza kupendekeza masuala ambayo ni muhimu kwako zaidi. Kwa hivyo, pia, habari kuhusu mahali unapoenda.

Kuwepo kwako katika baa fulani Ijumaa usiku au mahali pa ibada, kwa mfano, kunaweza kuwasilisha taarifa kuhusu mtazamo wako juu ya masuala fulani, ambayo ni muhimu kwa kampeni zinazoanzisha majukwaa ya kisiasa. Kwa kujua msimamo wako, wanaweza kuchagua kukulenga kwa ujumbe mahususi - au kukupuuza moja kwa moja.

Taarifa ya eneo si taarifa tu kuhusu mahali ulipo kwenye ramani. Pia inatoa picha ya kile unachopenda kufanya na unachovutiwa nacho. Aina fulani ya taaarifa ya eneo inatumiwa kulenga watu katika takriban kila kampeni za uchaguzi duniani kote.

Takriban kampeni zote hutumia majukwaa makubwa ya teknolojia kulenga matangazo (kulingana na mahali ulipo na unapoenda), iwe ni katika jiji fulani, wilaya, kitongoji, au hata kaya mahususi.

Kulenga kieneo kunaweza kuchukua aina nyingi, lakini aina tatu zinazojulikana zaidi ni:

  • Kuunda ‘wigo wa kieneo’ karibu na sehemu mahususi katika ulimwengu wa kweli (kama vile jengo au tukio mahususi) ambayo huchochea ujumbe wa kisiasa kuonekana wakati watu binafsi hupitia humo.
  • Kutambua takribani maeneo ya wapiga kura kulingana na anwani zao za IP (kikoa cha kimtandao)
  • Kwa kutumia taarifa za idadi ya watu, kama vile anwani ya posta, kulenga ujumbe wa kisiasa kwa wapiga kura

Sio tu kampuni zilizobobea katika huduma za kampeni za kisiasa ambazo hufanya aina hii ya ulengaji wa eneo. Kampuni zingine zinazokusanya au kupata taarifa za eneo zimejulikana kutoa taarifa hizo kwa vyama vya siasa. Kwa mfano, Programu ya The Weather Channel ilitoa maelezo ya eneo kwa ajili ya matangazo ya kisiasa, wakati Snapchat ni jukwaa maarufu kwa vyama vya siasa kuwalenga wapiga kura kwa matangazo kulingana na mahali walipo.

KIDOKEZO CHA 5: Weka Kikomo Nani Anayejua Ulipo

Je, unafikiria kuhudhuria mkutano wa kisiasa au maandamano, au kwenda tu kwenye kituo chako cha kupiga kura? Chukua hatua fulani dhidi ya ulengwaji kulingana na eneo kwa kudhibiti data ya eneo lako.

Futa nyayo za eneo lako kutoka kwa vifaa vyako vya rununu.


Naweza Kufanya Nini?

Fanya Sauti Yako Isikike

Ikiwa ungependa kufanya zaidi ili kudhibiti jinsi taarifa zako za faragha zinavyotumika katika uchaguzi, unaweza kusaidia kwa kueneza habari.

KIDOKEZO CHA 6: Zungumza

Zungumza au waandikie wawakilishi na vyama vya kisiasa katika eneo lako na waulize jinsi wanavyotumia data yako katika kampeni zao za kisiasa.

Iwapo unajali kuhusu utendaji fulani, kama vile uwekaji wasifu unaotegemea eneo kwa mfano, andikia au pigia simu wadhibiti wa uchaguzi ili kuwajulisha unavyohisi.

Onesha Msimamo Wako

Njia tata na zisizoeleweka ambazo teknolojia hizi za kampeni hutumiwa zinaweza kukufanya uzidi kuvunjika moyo na kutojihusisha na mojawapo ya michakato muhimu zaidi katika demokrasia - kitendo cha kupiga kura. Unapoelewa jinsi taarifa zako zinavyotumiwa kukushawishi katika uchaguzi, unaweza kufanya chaguo sahihi zaidi za kisiasa. Ikiwa unataka kuwawezesha wengine kufanya vivyo hivyo, sambaza neno.

KIDOKEZO CHA 7: Iambie Jumuiya Yako

Zungumza na marafiki na familia yako kuhusu jinsi taarifa zako (na zao) zinatumiwa wakati wa msimu wa kampeni na jinsi inavyoweza kubadilisha namna wanavyolengwa. Kadri watu wanavyojua zaidi na kadri uhamasishaji unavyofanywa kuhusu mada hii, ndivyo inavyojenga uwezekano wa kulishughulikia suala hili zaidi, kwa hivyo tafadhali shiriki mwongozo huu na wengine!

Ilisasishwa mara ya mwisho mnamo: 21/2/2023